Katika kusoma na kujufunza somo la Historia, wanafunzi wengi hupata shida kulielewa somo sababu ya lugha. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kujifunza na kuelewa Historia kwa wanafunzi wa Kidato cha kwanza. Lugha ambayo imetumika katika uandishi wa kitabu hiki ni nyepesi. Hivyo, mwanafunzi hatapata ugumu kuelewa maudhui yaliyomo katika kitabu hiki. Vilevile uandishi umezingatia kiwango cha ulewa wa mwanafunzi kwa kiwango hiki kwa kuandika sentensi fupifupi .
Kitabu hiki pia kitamsaidia mwalimu anapoandaa somo ili wanafunzi wake wapate ulewa uliyolengwa katika muhtasari wa somo la Historia kwa kidato cha kwanza.
Dkt . Ernesta Mosha
Mkurugenzi
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.