Jifunze Hisabati kidato cha kwanza ni kitabu cha Hisabati kwa shule za sekondari kilichaandikwa kwa kuzingatia muhtasari wa shule za swkondari nchini Tanzania.
Ni kitabu cha aina yake kwa kuwa kimetunia lugha ya taifa letu la Tanzania, Kiswahili. Kitabu hiki kimesheheni istilahi za taaluma ya Hisabati hivyo kukifanya kiwa na ‘ladha’ na mvuto wa pekee. Matumizi ya istilahi za kitaaluma katika kitabu hiki, yanatoa jibu kwamba “Inawezekana kufundisha masomo yote, katika viwango vyote vya elimu nchini kwa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili.”
Mada zimetolewa ufafanuzi wa kina kwa kutumia maelezo kuntu na lugha fasaha. Fauka ya hayo, kitabu hiki kimesheni mifano maridhawa katika kila mada kiasi cha kumfanya mwanafunzi au mtumiaji aweze kufuatilia na kujifunza Hisabati yeye mwenyewe bila hata msaada wa mwalimu wake.
Kila sura ya kitabu hiki ina mazoezi ya kutosha. Aidha, baada ya mada ndogo zina mazoezi ya kumsaidia mwanafuzi katika yale anayopaswa kujifunza. Mazoezi haya yatampa changamoto mwanafunzi na kufanya ajitume daima hivyo kujijengea umahiri na ufanisi katika somo la Hisabati. Vilevile katika kurasa za mwisho, kuna majibu ya mazoezi yote yaliyomo kitabuni. Kujihakiki kama yu sahihi au la.
Kwa kuwa kitabu hiki kimetumia lugha ya Kiswahili ambayo hueleweka vyema kwa wengi, hakuna mashaka kwamba, hesabu zitaeleweka barabara na kupendwa zaidi.
Dkt. Ernesta S. Mosha,
Mkurugenzi,
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.