UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU

Hili ni toleo la tatu la kamusi ya Kiswahili sanifu. Toleo la kwanza lilitolewa mwaka 1981. Toleo hilo lilikuwa kamusi ua kwanza ya maneno sanifu ya Kiswahili. Toleo lililofuata lilichaposhwa mwaka 2004. Oxford University press ndiyo mchapishaji wa matoleo yote matatu.

Uandishi wa toleo hili ni ushirikiano wa wanaleksikografia  na wataalamu wa lugha na fasihi wa taasisi ya taaluma za Kiswahili (TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( ambayo zamani ilijulikana TUKI)

Mbali na hao, wataalam wengine, wadau na wapenzi mbalimbali, ndani na nje ya Afrika Mashariki, wameshiriki katika kutoa maoni yao juu ya namna ya kuliboresha toleo hili la tatu la kamusi ya Kiswahili sanifu.

Nakala Zaidi ya milioni 2 zimeuzwa hadi sasaa

Kamusi hii ina historia ndefu. Ni miaka Zaidi ya 45 toka wazo la kuibuni, kuitunga, kuitafiti, kuichapa chapisho la kwanza, kuihakiki , kuidurusu, kuipanua, kuisanifu upya na kuiboresha.

Kamusi hii imewashughulisha watu wengi kwa miaka mingi katika kuitunga na kuiendeleza. Kwa kuidurusu utapata thibitisho tosha la kukua na kwenda kwake na wakati

Toleo hili la tatu lililoboreshwa lina :

  1. Maneno ya jumla Zaidi ya 285,000
  2. Maneno sanifu na yanayokubalika
  3. Vidahizo Zaidi ya 25,000 (vikiwemo vibadala na minyambuliko ya vitenzi)
  4. Vidahizo vipya vilivyoteuliwa, takriban 2,000
  5. Baadhi ya istilahi za Nyanja na taaluma mbalimbali
  6. Matamshi na hati za konetiki za kimataifa
  7. Ngeli zilizoainishwa kimolojia, kisintsksia na kisemantiki
  8. Etimolojia ya vidahizo
  9. Njia rahisi nay a haraka ya kutambua visawe, misemo, nahau, methali , n.k.
  10. Picha na michoro ya kuvutia Zaidi ya 1,150
  11. Kurasa 16 za michoro ya rangi kuhusu mada mbalimbali

KAMUSI INAYOAMINIKA KOTE DUNIANI: ISOME. IHAKIKI. ITUMIE.