Chapisho hili ni zao la ushirikiano kati ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) na Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA). Sura zilizomo katika chapisho hili zimetokana na Kongamano la CHAKAMA lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya mjini Thika (Kenya) mwaka 2015. Kongamano hilo lilihudhuriwa jna wajumbe kutoka maeneo mbaimbili duniani. Katika kongamano hili yaliibuka mambo mengi na muhimu kuhusu lugha ya Kiswahili na mustakabali wake ndani na nje ya Afrika mashariki. Kwa kuzingatia mwitikio wa hali ya juu wa washiriki wa kongamano na mada zilizowasilishwa katika kongamano hili waharirir waliona kuwa litakuwa jambo la welekevu kutoa vitabu viwili ambavyo ni Lugha ya Kiswahili: utafiti na maendeleo na Fasihi ya Kiswahili: utaditi na maendeleo. Toleo hili litawafaidisha wanataaluma wa ngazi mbalimbali kususani wahadhiri, wakufunzi na hata wapenzi na wasomaji wote wa Kiswahili. Hivyo tunawaalika wasomaji wetu na wapenzi wa lugha adhimu ya Kiswahili kusoma sura zilizomo katika toleo hili, kutafakri, kukosoa na kuboresha yaliyomo kwa manufaa ya maendeleo ya lugha hii na taaluma yake.
YALIYOMO:
- Hali ya Kiswahili nchini Rwanda. (Pacifique Malonga)
- Changamoto na mustakabali wa Kiswahili nchini Uganda. (Miima A. Florence na Vicent Kawoya)
- Tathimini ya tovuti ya swahilihub katika kuendeleza Kiswahili Kitaaluma. (Anthony Owino Oloo na Keneth Inyani Simala )
- Mchakato mpya wa kueneza dini kiutandawazi na athari zake katika mustakabali wa maenezi ya Kiswahili. ( Alex Umbima Kevego, Mwenda Mukuthuria na Ayub Mukhwana)
- Mchango wa mwaka kogwa katika kuuenezi na kuurndeleza utamaduni wa mmakunduchi na maswali (Musa M. Hans)
- Ruwaza za matumizi ya lugha katika bishara: mfano wa mji wa Eldoret. (Toboso Mahero Bernard na Mosol Kandagor)
- Nadharia za kisasa na uamili wa mofimu za Kiswahili kimofosintaksia. (Basilio G. Mungania)
- Nafasiya nadharia ya Myers-Scotton katika uchunguzi wa matokeo ya mitagusano ya lugha katika kiwango cha kimofosintaksia. (Susan Choge)
- Uchanganuzi wa uhamishaji wa mofosintaksia ya kiluo kwa Kiswahili. (Carolyne Oduor na Kenneth Inyani Simala)
- Matatizi ya ufafanuzi wa ‘maana’ katika leksikografia ya Kiswahili. (Nahashon A. Nyageri na Enock Matundura)
- Vyanzo vya kalosa ya kisemantiki katika mawasilino andishi ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Kenya. (Aruba B. Kemunto na James O. Ontieri)
- Usarufi na usemantiki wa uradidi. (Nelli V. Gromova)
- Sera ya lugha na matumizi ya Kiswahili nchini Kenya: haja ya mustakabali mpya. (Simiyu Kisurulia, Oyuma Oyondi na Arthur Muhia)
- Matumizi ya lugha katika mitandao ya kijamii: mfano wa Kiswahili katika blogu za kikristo. (Alex Umbima Kevogo na Stanley Adika Kevogo)
- Mikakati inayitumiwa na vyombo vya habari nchini Kenya kukabiliana na changamoto za kiistilahi. ( Stanley Adika Kevogo na Mwenda Makuthuria)
- Nafasi ya vyombo vya habari katika kudunisha Kiswahili nchini Kenya katika karne ya 21.(Jane K, Maithya)
- Ujitoshelezaji wa kiswahili kama chombo cha mawasiliano. (Ayub Mukhwana)
- Uchanganuzi wa matumizi ya lugha –ishara katika fasiri ya habari za kiswahili katika vituo vya Televisheni vya KTN na KBC. (Ellen Anyiso Otieno, Kenneth Inyani Simala na John Habwe)
- Matumizi ya teknolojia katika ufundishaji wa Kiswahili nchini Kenya. (Sikolia C. Kalabai)
- Tamthmini ya lugha ya kufundishia kuanzia shule za chekechea hadi darasa la tatu nchini Kenya. (Leonard Chacha na Judy Onyancha)
- Matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu Tanzania: ni ukombazi wa kiutamaduni ama mbio za kisiasa?. (Hadija Jilala)
- Matumizi ya lugha –ishara katika ufundishaji wa sarufi ya Kiswahili kwenye shule za msingi mkoani Nyanza, Kenya. (Ellen Anyiso Otieno, Kenneth Inyani Simala na Tobias M. Shikuku)