UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

UBINADAMU TABIA

Mwandishi Asha  Shabani Kibwana Kunemah alizaliwa tarehe 12, Mei 1948 huko Muheza, mkoani Tanga nchini Tanzania. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Masuguru iliyoko wilayani Muheza. Baadaye alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Wasichana Korongwe. Alisomea ualimu mkoani Tabora na kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wilayani Mafinga.

Aidha, aliwahi kuwa mwalimu na mwalimu mkuu katika shule mbalimbali kwa miaka 15 zikiwemo shule za msingi Boma na Zingibari. Baadaye aliteuliwa kuwa Afisa Elimu wa Sayansi kimu na Afya katika wilaya ya Pangani  kwa  miaka 12 hadi  alipostaafu  tena  katika  Chuo cha Ualimu  Msambazi kwa mkataba.

Bi. Asha na mumewe Bwana Kunemah, walifanikiwa kupata watoto sita. Kwa sasa ni mstaafu anayejishughulisha na uandishi  wa  vitabu.  Mbali na kitabu hiki, mwandishi amefanikiwa kuchapisha vitabu vifuatavyo:

  • Maana Zaidi ya Moja: Namba 1 na 2.
  • Mwana Pangani.
  • Misemo na Methali katika Ushairi, Toleo la 1 na 2.
  • Faridina  Fadina: Toleo la Kwanza.
  • Ubinadamu Tabia: Toleo la Kwanza.